Duration 8:16

Chakula Cha Kuku wa Kienyeji, Vifaranga na Kuku Wakubwa

19 796 watched
0
128
Published 3 Nov 2021

Chakula cha kuku wa Kienyeji, vifaranga wa kienyeji na kuku wanaotaga. Mfugaji wa kuku wa kienyeji nakushauri uwalishe kuku chakula kulingana na mfumo unaowafugia:- Kwa kuku wanaofugwa huria wanaweza wakapewa pumba na mabaki ya chakula cha nyumbani na bado wakatoa matunda mazuri (kuku wakubwa). Lakini pia unaweza ukawaongezea funza, Azolla au hydroponics fodder. Kwa kuku wanaofugwa nusu ndani nusu nje walishe hivi, chukua mfuko mmoja wa concentrate uchanganye na pumba gunia moja. Concentrate ni chakula ambacho kimetengenezwa kwa Malighafi mbalimbali ambazo ziko kwa kiwango kikubwa hivyo ni lazima uchangaye na pumba ili kupata uwiano wa virutubisho. Pia waongeze Azolla au hydroponics au funza ili wapate vitamin na Madini ya ziada. Ili Upate faida nzuri kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji haupaswi kutumia pesa nyingi kwenye Chakula cha kuku, gharama za chakula zikienda juu mfugaji wa kuku wa kienyeji hapati faida. Watumiaji wa Mfumo wa Huria kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji wanaweza kuchanganya Concentrate kilo 25 na Pumba kilo 100, na chakula hicho kikafaa kabisa kwaajili ya kuku na wakakupa mazao Mazuri.

Category

Show more

Comments - 17